Saturday, November 10, 2012
KUONGEZEKA KWA WACHEZAJI WAGENI NDIO KUMESABABISHA HALI KUWA TETE LIGI KUU NCHINI UINGEREZA - FRIEDEL.
GOLIKIPA wa zamani wa kimataifa wa Marekani ambaye ancheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs, Brad Friedel amesema kumekuwa na hali tete katika Ligi Kuu nchini Uingereza kutokana na kuongezeka kwa wachezaji wengi waa kigeni ambao wanatoka katika tamaduni tofauti. Friedel mwenye umri wa miaka 41 ambaye amecheza michezo 310 katika ligi kuu aliambia radio moj nchini Uingereza kuwa ligi hiyo imebadilika kwa kiasi kikubwa toka alipoanza kucheza nchini humo katika miaka ya tisini. Nyota huyo amesema kuwa soka limekuwa katika hali tete tofauti na miaka 20 iliyopita lakini katika kipindi hicho kulikuwa hakuna wengi wa kigeni kama ilivyokuwa hivi sasa. Friedel aliendelea kusema kuwa unapokubali kupokea watu kutoka sehemu tofauti na wenye tamaduni tofauti wanakuwa wamezoea kupokelewa kwa namna tofauti hivyo si kila tamaduni duniani mtu akimkosea mwenzake wanaweza kushikana mikono na kusahau yaliyotokea. Friedel ambaye amewahi kukipiga katika klabu ya Liverpool, Blackburn Rovers na Aston Villa kabla ya kuhamia Spurs June mwaka jana bado ni golikipa namba moja wa timu hiyo akigombea namba na rafiki yake Hugo Lloris ambaye ni golikipa wa Ufaransa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment