RATIBA ya michuano ya Kombe la Tusker kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA ambayo ilikuwa ipangwe Novemba 8 mwaka huu jijini Kampala imesogezwa mbele kwa siku nne zaidi. Michuano hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi Novemba 24 mpaka Desemba 8 jijini Kampala katika Uwanja wa Taifa wa Mandela uliopo Namboole ratiba yake sasa itapangwa Novemba 12. Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini Uganda-FUFA ambaye pia anafanya shughuli hiyo CECAFA, Rogers Mulindwa aliwaambia waandishi wa habari jijini Kampala mabadiliko ya tarehe hiyo bila kutoa maelezo zaidi ya sababu iliyopelekea kusogezwa mbele kwa uapngwaji huo wa ratiba. Wakati michuano hiyo ikianza Uganda haitakuwa ikitetea taji hilo pekee lakini pia kushinda taji kwa rekodi ya mara 13 toka michuano hiyo ianzishwe.
No comments:
Post a Comment