Wednesday, November 21, 2012
REKODI BINAFSI HAINA UMUHIMU KWANGU - MESSI.
Mshambuliaji wa Barcelona, LIONEL MESSI amesisitiza kuwa mawazo yake yapo katika kuisaidia timu yake kuliko kufikia rekodi ya kufunga mabao 85 katika kipindi cha mwaka mmoja aliyoweka GERD MULLER wa Ujerumani. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina aliifungia Barcelona mabao mawili na kuisadia timu yake hiyo kuifunga Spartak Moscow mabao 3-0 na kumfanya kufikisha mabao 80 kwa mwaka huu lakini Messi amesema mataji kwa timu yake ndio muhimu zaidi kuliko rekodi binafsi. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo kuhusiana na suala ya yeye kuikaribia rekodi ya MULLER, MESSI amesema kuwa kitu muhimu kwake ni timu yake kupata matokeo mazuri ndio maana amekuwa akifanya juhudi pamoja na wachezaji wenzake kuhakikisha hilo linawezekana. Naye kocha wa Barcelona TITO VILANOVA aliungana na MESSI akidai kuwa nyota huyo hachezi ili aweze kuvunja rekodi bali kuisaidia timu ili iweze kufanya vizuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment