KLABU ya Arsenal inaweza kupoteza kiasi cha paundi milioni 30 kwa mwaka wanazopata kutoka kwa wadhamini wao Emirates kama klabu hiyo ikishindwa kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Meneja wa klabu hiyo Arsenal Wenger ameiongoza kushiriki michuano hiyo kila msimu toka amechukua mikoba ya kuinoa ya kuinoa timu hiyo. Lakini hivi sasa Arsenal inakabiliwa na msimu mgumu chini ya kocha huyo Mfaransa na wako katika hatari ya kukosa taji lolote katika kipindi cha miaka nane mfululizo huku wakiwa bado wanapigania nafasi nne za juu ili washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Emirates wadhamini wa klabu hiyo ambao wako katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpaka msimu wa mwaka 2014-2015 wameamua kuionya klabu hiyo kwa kuchukua tahadhari kama ikishindwa kushiriki michuano ya klabu bingwa. Kwasasa Arsenal wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza lakini kuna uwezekano mkubwa wa kutoka katika nafasi hiyo kama Chelsea ambao walikuwa katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia iliyofanyika Japan wakishinda mechi zao mbili za viporo walizonazo.
No comments:
Post a Comment