Sunday, December 23, 2012

Lionel Messi ● All 91 Goals in 2012 ● New World Record


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amefunga bao la mwisho katika rekodi ya mwaka aliyoivunja wakati timu yake ikishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Valladolid jana usiku. Bao alilofunga Messi katika kipindi cha pili linamfanya kufikisha mabao 91 kwa mwaka huu baada ya kuipita rekodi iliyowekwa kwa kipindi cha miaka 40 na Gerd Muller aliyefunga mabao 85 mwaka 1972. Ushindi huo umeifanya klabu hiyo kujikita kileleni kwa tofauti ya alama tisa na Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya pili huku pia wakiwapita mahasimu wao Real Madrid wanaoshika nafasi ya tatu kwa alama 16. Katika mchezo huo timu zote mbili ziliingia uwanjani zikiwa na fulana maalumu zilizokuwa na ujumbe mahsusi kwa ajili ya kocha wao Tito Vilanova aliyefanyiwa upasuaji wa koo Alhamisi iliyopita.

No comments:

Post a Comment