Friday, December 28, 2012

MACLEISH KUINOA NOTTINGHAM FOREST.

MMILIKI wa klabu ya Nottingham Forest, Fawaz Al Hasawi raia wa Kuwait amemteua kocha wa zamani wa klabu ya Aston Villa Alex MacLeish kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ikiwa zimepita saa 24 toka amtimue aliyekuwa kocha wa timu hiyo Sean O’Driscoll. Al Hasawi amesisitiza kuwa alikuwa anataka kocha mwenye uzoefu wa Ligi Kuu nchini Uingereza wakati alipotoa uamuazi wa kushangaza kwa kumfukuza O’Driscoll kufuatia ushindi wa mabao 4-2 iliyopata timu hiyo dhidi ya Leeds United Jumatano. Tajiri huyo alifuata uamuzi wake kwa kumuajiri McLeish ambaye ameisaidia klabu ya Birmingham kupanda kutoka Ligi Daraja la Pili walipokuwa lakini alitimuliwa na Villa msimu uliopita baada ya kuifundisha kwa mwaka mmoja. Al Hasawi amesema amefanya uamuzi wa kumchukua McLeish kutokana na uzoefu wake wa ligi kuu hivyo anaamini atawasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea.

No comments:

Post a Comment