Friday, December 28, 2012

NIPO FITI - ABIDAL.

BEKI wa Barcelona Eric Abidal amesema anajisikia vyema na yuko tayari kurejea tena uwanjani ikiwa ni miezi nane imepita toka afanyiwe upasuaji wa kupandikizwa ini jingine. Akihojiwa Abidal mwenye umri wa miaka amesema ni muda mwingi umepita toka afanyiwe upasuaji na amekuwa akipambana ili aweze kurejea katika hali yake kawaida. Abidal alifanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini jingine April 10 ikiwa ni mwaka mmoja toka alipoondolewa uvimbe wa kansa katika ini lake Machi 2011. Beki huyo alianza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake Desemba 19 siku ambayo ndiyo taarifa za kocha wa klabu Tito Vilanova kurudiwa na tatizo la kansa ya koo zilipotangazwa. Vilanova naye alifanyiwa upasuaji mwingine wa kuondoa uvimbe huo wa kansa na baadae kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo kwasasa anaendelea na matibabu ya mionzi kwa kipindi cha wiki sita.

No comments:

Post a Comment