Friday, December 28, 2012

MEIRELES APUNGUZIWA ADHABU.

KIUNGO nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Fenerbahce, Raul Meireles amepunguziwa adhabu ya kufungiwa michezo 11 mpaka kubakia mchi nne kwa kosa la kumshambulia mwamuzi baada ya Shirikisho la Soka nchini Uturki kukata rufani. Tume iliyokuwa ikisimamia suala ilitumia muda wa saa sita kuangalia picha za video za tuko hilo wakati wa mchezo dhidi ya mahasimu wao Galatasaray uliofanyika Desemba 16 na kufikia muafaka kwamba nyota huyo wa zamani wa klabu za Chelsea na Liverpool alizozana na mwamuzi lakini hamkumtemea mate kama ilivyoonekana mara ya kwanza. Katika taarifa yake tume hiyo imesema wakati mchezaji huyo akiendelea kuongea muda wote wa tukio isingeweza kuwa rahisi kudhamiria kumtemea mate mwamuzi huyo. Meireles mwenye umri wa miaka 19 tayari alikuwa amefungiwa mchezo mmoja baada ya kupewa kadi mbili za njano katika mchezo dhidi ya Galatasaray na tume ilibadilisha uamuzi kwa kumtoza paundi 20,000.

No comments:

Post a Comment