Monday, December 10, 2012

PACQUIAO APUUZA USHAURI WA KUACHANA NA NGUMI ALIOPEWA NA MKEWE PAMOJA NA MAMA MZAZI.

BINGWA wa zamani wa ngumi duniani Manny Pacquiao amepuuza ushauri wa mama pamoja na mke wake wa kuachana na ngumi kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa mpinzani wake Juan Manuel Marquez wa Mexico. Pacquiao raia wa Philipines alipigwa kwa knock out katika raundi ya sita na Marquez katika pambano lisilokuwa la ubingwa lililofanyika Las Vegas, Marekani Jumamosi iliyopita. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 33 aliwasikiliza mke wake Jinkee na mama Dionisia wakilia kwa uchungu kutaka aachane na mchezo wa ngumi lakini Pacquiao amesema kuwa kwasasa atapumzika na baadae atarejea tena ulingoni. Akihojiwa na luninga moja nchini kwao Jinkee amesema huwa anapata wakati mgumu wakati anapomuona mumewe anapokea kipigo kama cha Jumamosi na siku zote amekuwa akimsisitiza kuachana na mchezo huo ili aweze kufanya mambo mengine ambayo anapenda. Lakini Pacquiao ambaye ameanza kucheza ngumi akiwa na umri wa miaka 16 amesisitiza kuwa kipigo hicho hakimaanishi kuwa uwezo wake wa kupigana umekwisha.

No comments:

Post a Comment