Monday, December 10, 2012
UNFORGETABLE NIGHT - FALCAO AKA THE TIGER
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Colombia na klabu ya Atletico Madrid, Radamel Falcao amesema kuwa hataweza kuusahau usiku wa jana baada ya kufunga mabao matano wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Deportivo la Coruna na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga idadi hiyo ya mabao katika La Liga katika muongo mmoja uliopita. Fernando Morientes ndiyo alikuwa mchezaji wa mwisho kufunga idadi hiyo ya mabao wakati akicheza katika klabu ya Real Madrid katika mchezo dhidi ya Las Palmas uliochezwa February mwaka 2002. Falcao aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa ni tukio la kipekee kufunga mabao matano katika mchezo wa ligi kwani anakumbuka mara ya mwisho alifunga idadi kama hiyo ya mabao wakati akiwa mdogo huko Bogota na kufunga mengine manne wakati akiwa Porto katika mchezo dhidi ya Villarreal lakini hakuwahi kufikisha matano akiwa mchezaji wa kulipwa. Nyota huyo amefikisha mabao 16 katika mechi 15 za La Liga msimu huu mabao matatu zaidi ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na mabao saba nyuma ya Lionel Messi wa Barcelona ambaye ndio anaongoza orodha ya wafungaji katika ligi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment