Thursday, January 31, 2013
ADEBAYOR AIPONDA CAF KUHUSU UWANJA WA MBOMBELA.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor amewabwatukia Shirikisho la Soka la Barani Afrika na Kamati ya Maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon kwa hali mbaya ya Uwanja wa Mbombela uliopo jijini Nelspruit. Adebayor ambaye anacheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza aliulalamikia uwanja huo kuwa na mchanga na mabonde baada ya Togo kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambapo watacheza na Burkina Faso Jumapili. Mbali na Adebayor, nahodha wa timu ya taifa ya Zambia Christopher Katongo naye alilalakia uwanja huo mapema wiki hii akidai kuwa inafanya timu yake ishinde kucheza mchezo wake wa kupasiana kama walivyozoea. Adebayor alidai michuano ya Afcon ni mikubwa barani Afrika na dunia nzima wanaangalia hivyo kuwa na viwanja vya aina hiyo ni jambo la kusikitisha. Nyota huyo amesema CAF lazima litafutie ufumbuzi suala hilo haraka ili wasiitie doa michuano hiyo ambayo mpaka sasa inaendelea vyema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment