Sunday, January 13, 2013

AFCON KUMPELEKA MPUTU ULAYA.

KIUNGO wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC, Tresor Mputu amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia katika vilabu vya Ulaya mara nyingi zaidi kuliko alivyofunga mabao kwa klabu yake na timu ya taifa. Mputu mwenye umri wa miaka 27 mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao zaidi ya 200 kwa timu yake ya taifa ya DRC na klabu ya TP Mazembe yenye maskani yake jiji la Lubumbashi lililo kusini mwa nchi hiyo. Zikiwa zimebakia siku chache kabla ya kuanza michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika nchini Afrika Kusini vyombo vya habari vimeanza tena kumfuatilia mchezaji huyo na kudai kuwa michuano hiyo itakuwa nafasi ya nyingine kwa nyota huyo kuonekana kwa vilabu vya Ulaya.  Vyombo vimeanza kutabiri kuwa kiwango alichonacho Mputu katika kukokota mpira pamoja na umahiri wa kufunga na kutengeneza mabao kitawavutia maskauti kutoka barani Ulaya ambao watakuwepo wakifuatilia kwa karibu michuano hiyo. 

No comments:

Post a Comment