Sunday, January 13, 2013

MOURINHO UNDER MORE PRESSURE.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho ameingia katika shinikizo zaidi jana wakati klabu hiyo ilipolazimishwa sare ya bila kufungana na klabu ya Osasuna ambayo inashika mkia matokeo ambayo yamewaacha nyuma kwa alama 15 mbele ya mahasimu wao Barcelona ambao wanaongoza La Liga. Katika mchezo Madrid ambao hawakutengeneza nafasi nyingi za kufunga walimkosa mshambuliaji wake nyota Cristiano Ronaldo ambaye alifunga mabao matano kati ya nane ambayo timu hiyo imeshinda katika michezo yake miwili iliyopita. Madrid sasa wanabakia katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 37 ikiwa ni alama nne nyuma ya Atletico Madrid wanaoshika nafasi ya pili ambapo pia kuna uwezekano wa kutofautiana na Barcelona kwa alama 18 kama timu hiyo ikishinda mchezo wake wa leo dhidi ya Malaga. Pamoja na matokeo hayo lakini Mourinho alikataa kuwalaumu wachezaji kwa kuwasifia kucheza vizuri na kufanya kila waliloweza kujaribu kufunga pamoja na kwamba hawakutengeneza nafasi nyingi.

No comments:

Post a Comment