Friday, February 22, 2013

CORINTHIANS HAIPASWI KULAUMIWA - RAIS.

RAIS wa klabu ya Corinthians ya Brazil, amesema kuwa kifo cha kijana wa miaka 14 kilichotokea wakati wa mchezo wao waliocheza nchini Bolivia kilikuwa ni bahati mbaya hivyo timu na mashabiki wake sio wakulaumiwa kutokana na tukio hilo. Kijana huyo Kevin Beltran raia wa Bolivia alifariki baada ya kupigwa na fataki usoni lililokuwa limerushwa na mmoja wa mashabiki wa Corinthians wakati wa mchezo wao wa Copa Libertadores uliochezwa Jumatano na kupelekea mashabiki 12 wa timu hiyo kukamatwa jijini Oruro. Rais wa klabu hiyo Mario Gobbi amesema kuwa hadhani kama Corinthians au mashabiki wake wanapaswa kulaumiwa kutokana na tukio hilo ambalo Shirikisho la Soka la Amerika Kusini limedai kuwa litafanyia uchunguzi. 
Waziri wa Michezo wa Brazil, Aldo Rebelo alitoa taarifa akiwa kuwa fujo za mashabiki hao hazikubaliki na kutaka mamlaka husika kuwapa adhabu wale wote waliohusika na vurugu hizo. 







No comments:

Post a Comment