Wednesday, February 20, 2013
PARALIMPIKI ITAENDELEA NA HARAKATI ZAKE - CRAVEN.
RAIS wa Kamati ya Kimataifa ya Paralimpiki, Sir Philip Craven amesema kuwa michezo ya watu wenye ulemavu itaendelea kama kawaida baada ya mshituko wa kukamatwa kwa Oscar Pistorius kutokana na kesi ya mauaji. Pistorius mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni bingwa mara mbili wa michuano ya paralimpiki alikana shitaka la kumuua kwa kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp katika nyumba yake nchini Afrika Kusini. Craven aliiambia BBC kuwa tukio hilo litakwisha baada ya muda na wataendelea na harakati zao za kuitangaza paralimpiki na kuwashawishi wanariadha zaidi waweze kushiriki. Waendesha mashitaka wanamtuhumu Pistorius kwa kumuua Steenkamp mwenye umri wa miaka 29 kwa makusudi ingawa mwanariadha huyo aliiambia mahakama hiyo kupitia wakili wake kuwa hakudhamiria kumuua mpenzi wake kwenye tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment