PISTORIUS APATA DHAMANA.
MWANARIADHA mlemavu Oscar Pistorius ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji ya rafiki yake wa kike amepewa dhamana baada ya kupita siku nne za usikilizaji wa kesi hiyo. Mwanariadha huyo ambaye ni bingwa wa michuano ya paralimpiki alikana tuhuma za mauaji akidai kuwa alimpiga risasi Reeva Steenkamp akidhani kuwa alikuwa jambazi. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea tena June 4 mwaka huu, ambapo alitozwa kiasi cha dola 74,000 kwa ajili dhamana yake huku akitakiwa kuwasilisha pasi yake ya kusafiria, kutorejea katika nyumba yake ya Pretoria na kuripoti polisi kila Jumatatu na Ijumaa. Hakimu aliyekuwa akisimamia kesi hiyo Desmond Nair alitumia muda wa saa mbili kutoa maamuzi yake lakini hakimu huyo pia alidai anapata wakati mgumu kuelewa kwanini Pistorius alivyatua risasi nyingi kiasi hicho.
No comments:
Post a Comment