SERIKALI IKO NUMA YENU - NAMWAMBA.
|
Ababu Namwamba. |
WAZIRI wa Vijana na Michezo nchini Kenya, Ababu Namwamba amelihakikishia Shirikisho la Soka la nchi hiyo-FKF kwamba serikali inawaunga mkono katika jitihada zao za kuomba kuandaa michuano ya Afrika kwa vijana itakayofanyika 2017 pamoja na Kombe la Mataifa ya Afrika-Afcon yatakayofanyika mwaka 2019. Akizungumza wakati wa sherehe za kumtambulisha kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Harambee Stars, Adel Amrouche waziri huyo amesema kuwa alimueleza rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF Issa Hayatou ni ya Kenya kutaka kuandaa michuano inayokuja walipokutana jijini Kampala. Namwamba aliendelea kudai kuwa mojawapo ya sheria za CAF ili nchi ipewe uenyeji wa kuandaa Afcon lazima iwe kwanza imeandaa mojawapo ya michuano ya vijana na wao wanataka kuanzia kwa kuandaa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17. Kenya inakabiliwa na changamoto nyingi haswa suala la miundo mbinu lakini waziri huyo alidai kuwa tayari wameshazungumza na nchi marafiki kama Qatar na China ambao wako tayari kuwasaidia kama wakipata nafasi ya kuandaa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment