Friday, March 8, 2013
AFUNGIWA MECHI 11 BAADA YA KUMVUNJA MWENZAKE MGUU HUKO UFARANSA.
KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Nice ya Ufaransa, Valentin Eysseric amefungiwa mechi 11 kwa mchezo m’baya aliocheza na kumvunja kifundi cha mguu mchezaji wa Saint-Etienne, Jeremy Clement mwishoni mwa wiki iliyopita. Eysseric na klabu yake wamethibitisha kuwa hawataka rufani kupinga adhabu hiyo iliyotolewa na tume ya nidhamu ya Ligi Kuu nchini Ufaransa na kumaanisha kuwa mchezaji huyo atakosa mechi zote zilizobakia msimu huu. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye amekuwa na msimu mzuri kwa kucheza katika kiwango cha juu alionyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa tukio hilo la kutisha alilofanya. Clement ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Olympique Lyon, Rangers na Paris Saint-Germain anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa kati ya miezi mitano na sita baada ya kufanyiwa upasuaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment