Friday, March 8, 2013

MISRI ITAFUZU KOMBE LA DUNIA 2014 - BRADLEY.

KIKOSI cha timu ya taifa ya Misri bado ina matumaini ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Qatar katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa jana. Qatar iliigaragaza Misri katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa jijini Doha kabla ya mchezo wao mgumu wa kufuzu michuano hiyo dhidi ya Zimbabwe utakaochezwa baadae mwezi huu. Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa Misri, Bob Bradley amesema matokeo hayo waliyopata hayamnyimi usingizi kwani bado kwani imani na wachezaji wake bado ipo na ana uhakika watafuzu Kombe la Dunia. Kikosi hico cha Bradley kinatarajiwa kucheza mchezo mwingine wa kirafiki Machi 22 na Swaziland kabla ya kukutana na Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment