Friday, March 8, 2013
NO PLAN B - VALCKE.
KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jerome Valcke amekiri kuwa hakuna mpango mwingine ulioandaliwa na kama Uwanja wa Maracana uliopo jijini Rio de Jenairo hautakuwa tayari kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika June mwaka huu. Uwanja huo mkongwe na maarufu nchini humo ambao ulitumika katika mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1950 upo katika matengenezo kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Kumekuwa na wasiwasi kwamba ujenzi wa uwanja unakwenda nyuma ya muda uliopangwa hususani kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jijini humo Jumanne na kupelekea baadhi ya sehemu kujaa maji na kulazimika wakaguzi wa FIFA kushindwa kuukagua. Maofisa wa FIFA wanatarajia kukutana na kamati ya maandalizi ya nchi hiyo, serikali ya jiji hilo na kampuni iliyopewa dhamana ya kuukarabati uwanja huo ili kujadili suala hilo. Valcke amesema hakutakuwa na mpango mbadala wowote kama Maracana au viwanja vingine vitano ambavyo vimeteuliwa kwa ajili ya michuano hiyo havitakuwa tayari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment