Thursday, March 7, 2013
BALLACK ATAKA SULUHU NA LOEW.
NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, michael Ballack amemualika kocha wan chi hiyo Joachim Loew na nahodha wa sasa Philipp Lahm katika mechi yake ya kuaga itakayofanyika jijini Leipzig June mwaka huu. Ballack amekuwa akikasirika jinsi soka lake la kimataifa lilivyoisha lakini kwa kuwaalika Loew na Lahm katika mchezo utakaozikutanisha timu ya marafiki wa mchezaji huyo na wachezaji wa kimataifa itakuwa ni ishara tosha ya kutaka usuluhishi. Uhusiano wa Ballack na Loew pamoja na Shirikisho la Soka la nchi hiyo ulikuwa umeingia utata baada ya kuchwa katika timu ya taifa ya nchi hiyo. Nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich, Chelsea na Bayer Leverkusen ambaye alitundika daluga rasmi Octoba mwaka jana pia alikataa mwaliko wa Loew wa kumuita katika kikosi cha timu hiyo ili aage katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Brazil. Lakini Ballack mwenye umri wa miaka 36 ambaye amefunga mabao 42 katika mechi 98 za kimataifa alizocheza amesema amekuwa katika mahusiano mazuri na Loew wakati bado hajastaafu soka la kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment