Wednesday, March 6, 2013
PSG, JUVE ZATINGA ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE.
KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kusubiria kwa miaka 18 wakati Juventus ambayo wamewahi kuchukua kombe hili mara mbili nao wametinga hatua hiyo baada ya miaka saba kupita. PSG ambao walicheza bila kiungo nyota waliomsajili hivi karibuni David Beckham walifanikiwa kutoka sare ya bao 1-1 na Valencia ya Hispania katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Parc des Princes na kupelekea kusonga mbele lwa jumla ya mabao 3-2. Huko jijini Turin, Juventus ambao wamewahi kuwa mabingwa wa michuano hiyo mwaka 1985 na 1996 wametinga katika hatua hiyo baada ya kuigaragaza Celtic ya Scotland kwa mabao 2-0 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0 katika michezo miwili waliyocheza. Mabao yaliyofungwa na Alessandro Matri katika kipindi cha kwanza na Fabio Quaglirella alilofunga katika kipindi cha pili yalitosha kuihakikishia nafasi Juventus ambao wanaongoza Ligi Kuu nchini Italia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment