Wednesday, March 6, 2013
BURKINA FASO YAMTIMUA KOCHA MSADIZI.
SHIRIKISHO la Soka nchini Burkina Faso limemtimua kocha msaidizi wa timu ya taifa ya nchi hiyo Sidi Napon baada ya kugombana na kocha mkuu Paul Put. Katika taarifa yake shirikisho hilo limedai kuwa wameshindwa kuvumilia tabia Napon ya kutomuheshimu mwenzake na wameamua kumuengua katika timu ya wakubwa na kumpa timu ya watoto. Meneja wa timu hiyo Gualbert Kabore naye pia alitimuliwa baada ya kuwatuhumu viongozi kutojumuisha jina lake katika orodha ya watu waliotunukiwa medali na rais wakiwemo wachezaji mara baada ya kurejea kutoka katika michuano ya Mataifa ya Afrika iliyofanyika nchini Afrika Kusini. Shirikisho hilo sasa limekabidhi majukumu yote Put ambaye ni raia wa Ubelgiji kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa kufuzu kwa mara kwanza michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil mwaka 2014 wakati wakitafuta watu wataoziba nafasi zilizoachwa wazi katika benchi la ufundi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment