Wednesday, March 6, 2013

FIFA YAIONYA DRC.

SHIRIKISHO la Soka la Dunia-FIFA limetuma barua rasmi kwa Wizara ya Michezo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC kuitaka kuondoa tarehe ya kuzitaka klabu zote nchini humo kucheza mechi zao za ligi katika viwanja vinavyomilikiwa na serikali. Wakosoaji na wachambuzi wa soka ndani ya nchi hiyo wanaamini kuwa tamko hilo linailenga klabu ya TP Mazembe ambayo mwaka jana ilifungua kituo chake binafsi cha michezo. FIFA limeitaka wizara hiyo ambayo inaongozwa na Banza Mukalay Nsungu kubadilisha uamuzi wake au wapewe adhabu ambayo inaweza kuathiri timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na vilabu vinavyoshiriki michuano iliyoandaliwa na Shrikisho la Soka barani Afrika-CAF. TP Mazembe ambayo ina maskani yake jijini Lubumbashi ilizindua uwanja wake mpya Juni mwaka jana ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 19,500, ukiwa ni mwa mmoja umepita toka wanunue ndege yao wenyewe yenye uwezo wa kubeba watu 140.

No comments:

Post a Comment