Thursday, March 7, 2013
TENISI KUTAMBULISHA MFUMO MPYA ILI KUWABAINI WADANGANYIFU.
SHIRIKISHO la Tenisi la Kimataifa-ITF linatarajia kutambulisha mfumo mpya wa pasi za kibaologia kwa wachezaji wa mchezo huo mwaka huu ili kusaidia kupambana na tatizo la utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu. Baadhi ya wachezaji wanaoshika orodha za juu kwa ubora wa mchezo huo duniani akiwemo Roger Federer wa Switzerland na bingwa wa michuano ya wazi ya Marekani Andy Murray wa Uingereza tayari wamezungumza kuonyesha kuunga mkono suala hilo ili kuulinda mchezo huo na wadanganyifu. Taarifa hizo zimekuja baada ya mkutano wa Kikundi cha Kupambana na Dawa za Kuongeza Nguvu katika Tenisi-TADP kilichokaa mapema wiki hii na kuwajumuisha wawakilishi kutoka ITF, ATP, WTA na grand slam tournaments. ITF imedai kuwa wamefikia hatua hiyo ili kuongeza juhudi za kuhakikisha mchezo wa tenisi unakuwa salama siku zote kwa kuepuka wachezaji wadanganyifu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment