Wednesday, March 6, 2013
BENDTNER AJUTIA KITENDO CHAKE KWA KUOMBA RADHI.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Denmark, Nicklas Bendtner ameonyesha masikitiko yake mahakamani baada ya kukutwa akiwa amelewa wakati akiendesha gari tukio ambalo limepelekea kufungiwa mechi za kimataifa. Mshambuliaji huyo wa Arsenal anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Juventus aliomba radhi kwa tukio hilo baada ya kufungiwa miezi sita kucheza mechi za kimataifa na Shirikisho la Soka nchini la nchi hiyo-DBU. Bendtner amefunga mabao 2 katika mechi za kimataifa 55 alizoichezea nchi yake lakini atakaa nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kukutwa na hatia ya kuendesha huku amelewa. Nyota huyo amesema mahakamani jijini Copenhagen kwamba anajutia kitendo hicho alichofanya na kudai kuwa ni mojawapo ya siku mbaya katika maisha yake na anajilaumu mwenyewe kwa alichofanya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment