Wednesday, March 6, 2013

SANAMU LA DHAHABU LA MGUU WA MESSI KUUZWA DOLA MILIONI 5 NCHINI JAPAN.

SANAMU la mguu wa kushoto wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi lililotengenezwa kwa dhahabu linatarajiwa kuingizwa sokoni baada ya kukamilika huko nchini Japan. Sanamu hilo lenye uzito wa kilo 25 na thamani ya dola milioni 5.25, limetengezwa kwa mfano wa mguu wa Messi na Ginza Tanaka ili kutambua rekodi ya nyota huyo kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara nne mfululizo. 
Kampuni hiyo ilidai kuwa sanamu hilo la dhahabu pamoja na matoleo ya vitu mbalimbali vitaingizwa sokoni ambapo sehemu ya mapato yake yataenda kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi na tsunami lililotokea miaka miwili iliyopita kupitia mfuko wa maalumu wa misaada unaoendeshwa na familia ya nyota huyo. Messi alinyakuwa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya nne katika sherehe zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA jijini Zurich, Switezerland Januari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment