Wednesday, March 6, 2013

CHAVEZ ALIKUWA NA NDOTO ZA KUCHEZA BASEBALL.

ALIYEKUWA rais kipenzi cha wananchi wa Venezuela, Hugo Chavez angeweza kuwa mchezaji wa baseball badala ya kuwa mwanasiasa kama sio majeruhi yaliyosababisha asitishe kucheza mchezo huo. Chavez, ambey amefariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 58 baada ya kupambana na kansa kwa karibu mwaka mmoja hakusita kuonyesha mapenzi yake kwenye mchezo huo unaopendwa zaidi nchini Marekani pamoja na mahusiano yasiyo ya kuridhisha aliyokuwa nayo dhidi ya taifa hilo. Katika mahojiano yake aliyofanya na mtangazaji maarufu wa CNN, Larry King mwaka 2009, Chavez amesema alijiunga na jeshi akiwa na umri wa miaka 17 kwa ajili kucheza baseball lakini majeruhi yalikatisha ndoto zake za katika mchezo huo. Chavez alisema ilikuwa ni ndoto zake kuwa nyota wa baseball na kucheza katika timu ya San Francisco Giants ya nchini Marekani lakini anadai mungu hakumpangia hivyo ndio maana ameishia kuwa mwana siasa baada ya kuachana na jeshi. Kwa mujibu wa kocha wa timu ya taifa ya baseball ya nchi hiyo, Luis Sojo amedai mara nyingi Chavez kuzungumzia mbinu zinazotumiwa na timu hiyo katika mashindano mbalimbali ya kimataifa hiyo inaonyesha jinsi gani alivyokuwa na mapenzi na mchezo huo.

No comments:

Post a Comment