Friday, March 29, 2013

FERDINAND ASHANGAZWA NA MASHABIKI WA UINGEREZA.

BEKI wa klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand ameonyesha kushangazwa na tukio la kibaguzi la mashabiki wa soka wa Uingereza lililomlenga yeye pamoja na ndugu yake Anton wakati wa mechi dhidi ya San Marino ambayo nchi hiyo ilishinda kwa mabao 8-0. Mashabiki hao ambao walikuwa wakipiga kelele za nyani kuwalenga Rio ambaye alijitoa katika kikosi cha Uingereza kutokana na maumivu ya mgongo na ndugu yake Anton ambaye anacheza katika klabu ya Queens Park Rangers-QPR. Ferdinand aliandika katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa twitter akielezea kusikitishwa kwake na kitendo hicho haswa kutoka kwa mashabiki wan chi yake mwenyewe. Rio amekuwa katika maelewano yasiyo mazuri na baadhi ya wachezaji wa Uingereza toka ndugu yake Anton afanyiwe vitendo vya kibaguzi na nahodha wa zamani wa Uingereza John Terry.

No comments:

Post a Comment