Friday, March 29, 2013

PISTORIUS KUSHIRIKI MICHUANO YA DUNIA JIJINI MOSCOW.

WAKALA wa mwanariadha mlemavu, Oscar Pistorius amesema mteja wake huyo anaweza kushiriki michuano ya riadha ya Dunia itakayofanyika jijini Moscow baada ya mwaka huu. Pistorius mwenye umri wa miaka 26 ambaye alikimbia katika michuano ya Olimpiki na Paralimpiki jijini London mwaka jana ameshitakiwa kwa kosa la kumuua rafiki wake wa kike lakini ataruhusiwa kusafiri baada ya mawakili wake kupinga baadhi masharti ya dhamana aliyopewa. Wakala huyo Peet van Zyl amesema kama atakuwa yuko tayari na kufuzu, basi hakuna shaka atshiriki michuano hiyo ya dunia itakayofanyika Agosti. Pistorius ambaye anatumia miguu ya bandia katika kukimbia anatuhumiwa kumuua rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp ambaye alipigwa risasi na kufa nyumbai kwake Februari 14 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment