Friday, March 29, 2013

UEFA KUTANGAZA ZABUNI KWA MIJI ITAKAYOTAKA KUANDAA EURO 2020, APRIL 16.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limefikia makubaliano ya kufanya zabuni ya mahitaji na sheria zitakazotumika katika michuano ya Ulaya 2020 abayo kwa mara ya kwanza itafanyika katika miji 13 tofauti itakayochaguliwa Septemba mwaka 2014. Katibu Mkuu wa UEFA Gianni Infantino aliviambia vyombo vya habari mara baada ya mkutano ulifanyika jijini Sofia kuwa wamefikia uamuzi wa kutangaza zabuni kwa mahitaji na sheria zitakazotumika kuanzia Aprili 16 mwaka huu. Waombaji watatakiwa kuwasilisha maombi yao ifikapo Aprili 25 ambapo UEFA itapitia zabuni zote katika kipindi cha Mei na Agosti na kuchagua miji 13 ifikapo Septemba mwakani. Mji 12 ambazo zitashinda zabuni hiyo zitapata nafasi ya kuandaa mechi tatu za hatua ya makundi pamoja na mechi moja ya hatua ya timu 16 bora au robo fainali wakati mji uliobakia wenyewe utapata nafasi ya kuandaa mechi mbili za nusu fainali pamoja na fainali.

No comments:

Post a Comment