Sunday, March 10, 2013
MESSI AWEKA HISTORIA KWA KUFUNGA MABAO KATIKA MECHI 17 MFULULIZO.
MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona Lionel Messi amekuwa mchezaji pekee katika historia ya soka kufunga mabao katika mechi 17 mfululizo kufuatia bao lake alilofunga katika Uwanja wa Camp Nou jana usiku katika mchezo dhidi ya Deportivo La Coruna. Bao la mshambuliaji huyo ambalo alifunga katika dakika za lala salama lilipelekea timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Deportivo na kupelekea nyota huyo kuweka rekodi mpya kwa kumpita Teotor Peterek aliyefunga mabao katika mechi 16 mfululizo. Peterek aliweka rekodi ya kufunga mabao 22 katika mechi 16 mfululizo za ligi daraja la kwanza nchini Poland katika msimu wa mwaka 1937-1938. Messi ambaye ameshafikisha mabao 200 katika La Liga, tayari ameshafunga mabao 40 katika ligi kuu msimu huu amabao ambayo yanaweza kumtosha kumfanya ashinde tuzo ya mfungaji bora wa ligi hiyo. Nyota wa zamani wa kimataifa wa Brazil ndio aliyekuwa akishikilia rekodi katika klabu hiyo ya kufunga mabao mfululizo katika mechi 10 katika kipindi akiwa Barcelona lakini Messi alishaipita rekodi zamani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment