Sunday, March 10, 2013

ROONEY KUONGEZWA MKATABA OLD TRAFORD.

MENEJA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema mshambuliaji wake Wayne Rooney ataongezwa mkataba mpya na klabu hiyo kabla ya mkataba wake wa sasa ambao analipwa kiasi cha paundi 230,000 haujamalizika 2015. Ferguson alitoa kauli hiyo ili kuondoa fununu juu ya mustakabali wa nyota huyo huko mbele baada ya kumuacha katika kikosi chake cha kwanza katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid uliochezwa katika dimba la Old Traford. Ferguson amesema hakuna suala la kuongea kuhusu mkataba wa Rooney kwani ukifikia wakati wa kuhitaji kuongeza itafanyika, hivyo hakuna la kuhofia kuhusiana na hilo. Pamoja na kusema hivyo lakini Ferguson anategemea kupungumza mshahara wa nyota huyo wakati wa kipindi cha mazungumzo ya mkataba mpya kama hataendelea kuwa chaguo la kwanza katika mechi kubwa.

No comments:

Post a Comment