Thursday, March 21, 2013

MWANARIADHA NGULI WA ZAMANI WA MBIO FUPI AFARIKI DUNIA.

MWANARIADHA nyota wa zamani wa mbio fupi kutoka Italia Pietro Mannea ambaye pia alikuwa akishikilia rekodi ya zamani ya mbio za mita 200 amefariki dunia akiwa na miaka 60. Mennea alishinda medali ya dhahabu ya mbio za mita 200 katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika jijini Moscow mwaka 1980 akimshinda bingwa wa mbio za mita 100 kutoka Uingereza Alan Wells aliyeshika nafasi ya pili. Mkongwe huyo alivunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 200 Septemba mwaka 1979 ambapo alitumia muda wa sekunde 19.72 rekodi ambayo ilidumu kwa kipindi cha miaka 17 mpaka ilipokuja kuvunjwa na Michael Johnson mwaka 1996 ambaye alikimbia kwa kutumia muda wa sekunde 19.66. Rekodi ya Johnson ambaye ni raia wa Marekani ilikuja kuvunjwa na Usain Bolt kutoka Jamaica katika michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini Beijing mwaka 2008 akitumia muda wa sekunde 19.19 lakini muda aliotumia Mennea unabakia katika rekodi za Ulaya. Rais wa Kamati ya Olimpiki nchini Italia Giovanni Malago amesema mwili wa Mennea utazikwa katika makao makuu ya kamati hiyo. Hakuna chanzo chochote kilichotajwa kusababisha kifo cha nguli huyo.

No comments:

Post a Comment