Thursday, March 21, 2013

NI MMOJA AU WAWILI KUTOKA BARCELONA NA MADRID NDIO WANGEFAA BAYERN - HOENESS.

RAIS wa klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani, Uli Hoeness anaamini kuwa wachezaji wawili au watatu kutoka Barcelona na Real Madrid ndio wanaweza kucheza katika kikosi cha kwanza cha vinara hao wa Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Bundesliga. Timu hizo mbili kutoka Hispania ndio zinaonekana kuwa na nguvu katika soka duniani kwasasa lakini Hoeness anafikiri Bayern na wenyewe wanaweza kujumuishwa huko kutokana na kikosi imara walichokuwa nacho. Akihojiwa ni wachezaji gani wa Barcelona ambayo angeweza kuwasajili katika kikosi cha Bayern kama angepata nafasi hiyo alimtaja Andres Iniesta na Jordi Alba. Bayern wamekuwa wakihusishwa na kutaka kufanya usajili wa majina makubwa kufuatia kutangaza kuwa Pep Guardiola anatarajiwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo msimu ujao lakini wamekataa kutaja aiana ya wachezaji watakaowahitaji katika kipindi cha majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment