Tuesday, April 16, 2013

11 WATEULIWA KUGOMBEA TUZO YA MARC VIVIEN FOE.

WACHEZAJI 11 wa Afrika wanaocheza katika ligi mbalimbali barani Ulaya wameteuliwa kugombania tuzo ya Marc-Vivien Foe ambayo kwasasa inashikiliwa na mchezaji wa kimataifa wa Morocco Younes Belhanda. Tuzo ya Marc Vivien Foe ilianzishwa mwaka 2009 kwa heshima ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon ambaye alianguka wanjani na kufa mwaka 2003 wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya nchi hiyo na Colombia mchezo ambao ulifanyika jijini Lyon, Ufaransa. Wachezaji walioteuliwa mwaka huu pamoja na vilabu na nchi wanazotoka ni pamoja na Aymen Abdennour-(Tunisia, Toulouse) Kossi Agassa (Togo, Stade de Reims) Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon, Saint-Etienne) Andre Ayew (Ghana, Olympique Marseille) Foued Kadir (Algeria, Olympique Marseille) Wahbi Khazri (Tunisia, Bastia) Saber Khelifa (Tunisia, Evian) Nicolas Nkoulou (Cameroon, Olympique Marseille) Jonathan Pitroipa (Burkina Faso, Stade Rennais) Alaixys Romao (Togo, Olympique Marseille) Alain Traore (Burkina Faso, FC Lorient) 
Washindi waliopita kuanzia mwaka 2009 ni Marouane Chamakh (Morocco, Bordeaux) , 2010 – 11 Gervinho (Ivory Coast, Lille – former club) na mwaka jana Younes Belhanda (Ivory Coast, Montpellier).

No comments:

Post a Comment