Tuesday, April 16, 2013

WAWILI KUPANDISHWA KIZIMBANI VURUGU ZA WEMBLEY.

WATU wawili wameshitakiwa bada ya vurugu zilizoibuka katika Uwanja wa Wembley wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA kati ya timu ya Millwall na Wigan Athletic. Vurugu zilizuka katika eneo walipokuwa mashabiki wa Millwall wakati timu yao ilipofungwa mabao 2-0 na Wigan katika mchezo huo. Mmoja kati watu hao mwenye umri wa miaka 43 ameshitakiwa kwa kuchochea vitendo vya kibaguzi wakati mwenzake mwenye umri wa miaka 53 yeye ameshitakiwa kwa kukiuka masharti ya dhamana. Ofisa Mkuu wa Upelelezi anayefuatilia kesi hiyo, Andy Barnes amesema vurugu zilizotokea katika mchezo huo ambao ulichezwa mwishoni mwa wiki iliyopita haziwezi kuvumiliwa kamwe. Barnes amesema uchunguzi utaendelea ili kuwabaini na wengine waliohusika katika vurugu hizo ili wafikishwe katika mkono wa sheria.

No comments:

Post a Comment