Thursday, April 18, 2013

BARCELONA KUANZA MAZUNGUMZO NA NEYMAR JULAI.

KLABU ya Barcelona imeonekana kukaribia kumnyakuwa nyota wa klabu ya Santos, Neymar baada ya klabu hiyo kupanga kuanza kufanya mazungumzo naye Julai mwaka huu. Neymar mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akisisitiza kuwa anataka kubakia katika klabu yake ya Santos mpaka baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 lakini amekuwa akipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kwamba atapata uzoefu wa kutosha barani Ulaya kama akienda mapema. Wachezaji wa Barcelona ambao ni raia wa Brazil, Dani Alves na Adriano wamekuwa wakimshauri nyota huyo kufanya uamuzi sahihi kwa kujiunga na klabu hiyo hivyo kuongeza chachu ya nyota kumwaga wino hapo. Neymar ambaye atakuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika Juni mwaka huu atasafiri kwenda Hispania muda mfupi baada ya kumalizika kwa michuano hiyo ili kuzungumzia mustabali wake.

No comments:

Post a Comment