Thursday, April 18, 2013

LIBYA YATENGA KIASI CHA DOLA MILIONI 314 KWA AJILI YA UJENZI WA VIWANJA.

WAZIRI Mkuu Msaidizi wa Libya Awad Ibrahim Elbarasi amesema serikali ya nchi hiyo imepanga kuwekeza kiasi cha dola milioni 314 kwa ajili ya ujenzi wa viwanja mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2017 kwa mategemeo kwamba michuano hiyo itawaunganisha wananchi baada ya vita ya mwaka 2011. Elbarasi amesema kama ilivyokuwa kwa Nelson Mandela alivyofanya nchini Afrika Kusini ni mategemeo yao wataiunganisha Libya kwa kutumia michuano hiyo. Waziri huyo aliendelea kusema kuwa ujenzi kwa ajili ya viwanja hivyo vipatavyo 11 unatarajiwa kuanza Juni mwaka huu na tayari fedha hizo zimekwishaombwa serikalini. Mwezi uliopita Libya ilidai kuwa itatumia rasilimali zake zote kuhakikisha wanalinda haki yao ya kuandaa michuano ya 2017 baada ya kushindwa kuandaa michuano ya Afrika ya mwaka huu na vita.

No comments:

Post a Comment