
Thursday, April 18, 2013
BUTT AAPA KUENDELEA NA KRIKETI.
NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya kriketi ya Pakistan, Salman Butt ameapa kuendelea kucheza mchezo huo pamoja na kushindwa rufani yake ya kupunguza adhabu ya kufungiwa. Butt mwenye umri wa miaka 28 alifungiwa miaka 10, na kuhitajika kuitumikia mitano huku mingine mitano ikisubiri kama atarudia kosa baada ya kukutwa na hatia ya kupanga matokeo mwaka 2011. Akihojiwa Butt amesema tayari ameshatumikia miaka miwili na miezi nane na baada ya miaka mingine miwili na miezi minne anaweza kurejea uwanjani tena. Butt na mchezaji mwenzake Mohammad Asif walishindwa rufani zao katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS jana ambapo Asif yeye amefungiwa miaka saba na miwili kati ya hiyo ikisubiri kama akirudia kosa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment