Thursday, April 18, 2013

BARCELONA KUFANYA ZIARA MALAYSIA.

MKURUGENZI Mtendaji wa klabu ya Barcelona, Antoni Rossich ametangaza kuwa klabu hiyo itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wachezaji nyoya wa Malaysia katika Uwanja wa Bukit Jalil abao una uwezo wa kuingiza mashabiki 100,000. Rossich akiwa sambamba na makamu wa rais wa Shirikisho la Soka nchini humo Prince Abdullah Ibni Sultan Haji Ahmad Shah amesema mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Agosti 10 mwaka huu jijini Kuala Lumpur. Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Barcelona kufanya ziara nchini Malaysia ambapo watakutana na kikosi kinachonolewa na kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo K. Rajagopal. Barcelona ambayo inanolewa na Tito Vilanova tayari imetangaza mipango ya kucheza mechi zingine za kujipima nguvu nchini China Agosti 3 na Thailand Agosti 7 katika ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

No comments:

Post a Comment