Thursday, April 18, 2013

RWANDA ITABAKIA KUWA SEHEMU MUHIMU KATIKA MAISHA YANGU - MICHO.

ALIYEKUWA kocha wa timu ya taifa ya Rwanda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ amesema nchi hiyo itabakia kuwa sehemu muhimu katika maisha yake pamoja na kutimuliwa kibarua chake jana. Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Ferwafa jana lilitangaza kukatisha mkataba na kocha huyo kutokana na matokeo yasiyo yakuridhisha ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata. Hivi sasa Micho mwenye umri wa miaka 43 ambaye mkataba wake ulikuwa umelizike Octoba mwaka huu anafanya kazi na washauri wake wa kisheria pamoja na Ferwafa kuangalia jinsi ya kulipwa stahiki zake. Lakini Micho alisisitiza kuwa pamoja na kutoa hayo lakini soka la nchi hiyo wananchi wake pamoja na watu wote aliofanya nao kazi watabakia sehemu muhimu katika maisha akiwa hapo kuanzia mwaka 2011 alipochukua mikoba ya Sellas Tetteh.

No comments:

Post a Comment