Saturday, April 27, 2013
DEL BOSQUE AALIKWA KONGAMANO LA CAF.
KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vincente del Bosque atarajiwa kuwa mgeni wakati wa kongamano lililoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF mwezi ujao jijini Cairo, Misri. CAF imeandaa kongamano hilo kwa kuwashirikisha wataalamu kwa lengo la kutathmini michuano ya Mataifa ya Afrika iliyofanyika nchini Gabon na Equatorial Guinea mwaka 2012 na ile ya Afrika Kusini iliyofanyika mwaka huu. Shirikisho hilo limedai kuwa lengo kubwa la kongamano hilo litakafanyika kuanzia Mei 11 mpaka 13 ni kuchambua mbinu za kiufundi katika michuano hiyo miwili iliyopita na kuangalia mapungufu yake ili waweze rekebisha au kuboresha zaidi katika michuano ijayo. Kwa mujibu wa maofisa wa CAF Del Bosque ambaye ameshinda Kombe la Dunia 2010 na Kombe la Ulaya mwaka 2012 akiwa na Hispania anategemewa kubadilishana uzoefu wake mkubwa alionao katika mkutano huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment