Wednesday, April 24, 2013
LEOZ AJIUZULU UJUMBE FIFA.
MJUMBE wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Nicolas Leoz kutoka Paraguay amejiuzulu wadhifa wake huo kutokana na kile alichodai kuwa na matatizo ya kiafya ikiwa ni siku chache kabla ya shirikisho hilo halijatangaza uchunguzi wa bakshishi katika michuano ya Kombe la Dunia. FIFA ilithibitisha kupokea barua ya Leoz mwenye umri wa miaka 84 ambaye pia ataachia ngazi wadhifa wake wa urais wa Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-CONMEBOL. Leoz ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo mara kadhaa amekuwa mjumbe katika bodi ya FIFA kuanzia mwaka 1998 na amekuwa rais wa CONMEBOL kuanzia mwaka 1986. Katika barua yake Leoz amesisitiza kuwa uamuzi aliochukua ni binafsi kutokana na matatizo ya kiafya aliyonayo kwani hawezi kusafiri mara tano kwa mwaka kama ilivyokuwa zamani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment