
Wednesday, April 17, 2013
MMILIKI WA CARDIFF KUTENGA KITITA CHA PAUNDI MILIONI 25 KWA AJILI YA MSIMU MPYA WA LIGI KUU 2013-14.
MMILIKI wa klabu ya Cardiff, Vincent Tan amesema klabu hiyo itatumia kiasi cha paundi milioni 25 kwa ajili ya maandalizi yao baada ya kupanda kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao. Cardiff ilitoa sare ya bila ya kufungana katika mchezo dhidi ya Charlton jana matokeo ambayo yaliirudisha klabu hiyo katika ligi kuu baada ya kukosekana kwa kipindi cha miaka 51. Tan amesema kwasasa wanatakiwa wajipange vizuri na wangependa kutumia fedha kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chao ili kiweze kuwa cha ushindani zaidi msimu ujao. Cardiff sasa wanaweza kushinda taji la ligi darajala kwanza kama wakifanikiwa kuwafunga Burnley ambao wanasota mkiani katika mchezo wa Jumamosi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment