Wednesday, April 17, 2013

ROY HODGSON AONYA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson ameonyesha wasiwasi wake kwa timu hiyo kutokana na kiu ya vilabu vya Ligi Kuu nchini humo kusajili wachezaji kutoka nje ya nchi. Hodgson amesema ana wasiwasi kwa wachezaji wazawa kushindwa kupata nafasi katika vilabu vikubwa nchini humo kutokana na vilabu hivyo kutafuta wachezaji nje badala ya kutengeneza vipaji walivyonavyo nchini humo. Kocha huyo amesema kuna baadhi ya mechi alizokwenda za ligi kuu anakuta hazina wachezaji wazawa hivyo hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kuinusuru nchi hiyo. Kwasasa mbili ya tatu ya wachezaji wa Ligi Kuu nchini Uingereza sio wazawa wa nchi hiyo na ni mojawapo ya ligi yenye wachezaji wengi zaidi wa kigeni barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment