KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amemuita golikipa Iker Casillas na mshambuliaji Fernando Torres katika kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitaanza maandalizi ya Kombe la Shirikisho linalotarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Brazil. Orodha hiyo ya wachezaji 26 itapunguzwa na kufikia 23 baada ya mzunguko wa mwisho wa mechi za Ligi Kuu nchini Hispania mwishoni mwa wiki ijayo. Hispania ambao ni mabingwa wa Dunia na Ulaya wana mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Haiti Juni 8 na Ireland siku tatu baadae kabla ya kuelekea nchini Brazil. Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Hispania imepangwa katika kundi B sambamba na Uruguay, Tahiti na Nigeria ambapo mchezo wa ufunguzi utachezwa Juni 16 dhidi ya Uruguay. Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu nane inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 15 mpaka 30.
Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), Victor Valdes (Barcelona), Pepe Reina (Liverpool)
Defenders: Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Jordi Alba (Barcelona), Ignacio Monreal (Arsenal), Raul Albiol (Real Madrid), Javi Garcia (Manchester City)
Midfielders: Javi Martinez (Bayern Munich), Xavi (Barcelona), Andres Iniesta (Barcelona), Sergio Busquets (Barcelona), Santi Cazorla (Arsenal), Xabi Alonso (Real Madrid), Benat Etxebarria (Real Betis)
Forwards: Cesc Fabregas (Barcelona), David Villa (Barcelona), David Silva (Manchester City), Roberto Soldado (Valencia), Pedro (Barcelona), Juan Mata (Chelsea), Jesus Navas (Sevilla), Fernando Torres (Chelsea).
No comments:
Post a Comment