Wednesday, May 1, 2013

DORTMUND WAKATA TIKETI YA KWENDA WEMBLEY.

KLABU ya Borussia Dortmund imefuzu katika fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika historia yao, licha ya kufungwa na Real Madrid mabao 2-0katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali. Dortmund waliishinda Madrid kwa jumla ya mabao 4-3, baada ya ushindi wao wa mabao 4-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza. Madrid waliingia uwanjani huku wakiitaji muujiza mkubwa wa kubadilisha matokeo baada ya kichapo cha wiki iliyopita, na kuanza kushambulia kwa kasi lango la wapinzani wao ambapo Gonzalo Higuain, Cristiano Ronaldo na Mesut Ozil walipoteza nafasi za wazi katika kipindi cha kwanza. Bao la kuongoza la Madrid lilifungwa katika dakika ya 83 na Benzema ambaye alimalizia pasi safi iliyopigwa na Ozil na bao la pili lilifungwa dakika sita baadae na nahodha Sergio Ramos lakini ushindi huo haukutosha kuivusha timu hiyo kwenye fainali ambayo itafanyika katika Uwanja wa Wembley Mei 25 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment