Wednesday, May 1, 2013

YES WE CAN - PIQUE.

IKIWA hata mashabiki wa Barcelona wanajua kuwa nafasi ya timu yao kugeuza matokeo ya mabao 4-0 waliyofungwa na Bayerm Munich katika mchezo wa kwanza kuwa ni ndogo, beki wa klabu hiyo Gerard Pique amesisitiza kuwa kikosi chao ndio pekee kinachoweza kufanya maajabu katika mchezo huo. Ni vilabu vitatu pekee ndivyo vilivyoweza kupata ushindi waliohitaji baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao mengi kwenye mchezo wa kwanza, mojawapo ikiwa ni mahasimu wa Barcelona, Real Madrid ambao walifanikiwa kushinda baada ya kufungwa mabao 5-1 na Borussia Moenchengladbach katika Kombe la UEFA msimu wa 1985-1986. Hatahivyo akihojiwa kabla ya mchezo wa leo wa marudiano katika uwanja wa Camp Nou Pique amesisitiza kuwa hakuna litakaloshindikana siku ya leo kwani watapigana kufa na kupona kuhakikisha wanapata nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo. Pique amesema wakati anapoingia uwanjani na kumuona Lionel Messi, Xavi Hernandez, Cesc Fabregas na Andres Iniesta huwa najiamini kwamba wanaweza kufanya lolote na kuipa ushindi timu yao.

No comments:

Post a Comment