Saturday, May 25, 2013

FA KUTAFUTA NAFASI YA KUANDAA MICHUANO YA ULAYA 2020.

MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Soka nchini Uingereza-FA, David Gill amekiri kuwa chama hicho kinajipanga kutuma maombi ya kuwa mwenyeji wa mchezo wa nusu fainali na fainali ya michuano ya Ulaya 2020. Gill ambaye alistaafu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa klabu ya Manchester United aliyoitumikia kwa miaka 10, alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA jana na sasa amepanga kuiongoza FA kuandaa fainali za 2020 ambazo zitachezwa katika nchi 12 tofauti barani Ulaya. Gill mwenye umri wa miaka 55 anaamini fainali ya leo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika Uwanja wa Wembley kati ya Bayern Munich na Borussia Dortmund itakuwa mfano tosha wa kwanini Uingereza ni sehemu salama kwa ajili ya mechi kubwa za Ulaya. Amesema Wembley ni mojawapo ya viwanja vikubwa kabisa katika ulimwengu wa soka hivyo bila shaka anaamini FA watatoa upinzani mkali katika kutafuta mwenyeji wa mechi hizo za Ulaya 2020.

No comments:

Post a Comment